DC KINONDONI AMTEMBELEA MUFTI MKUU WA TANZANIA OFISINI KWAKE

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abuubakar Zubeir.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi Mufti akizungumza na Sheikh Mkuu wa Tanzania Shekhe Abuubakar Zubeir.
DC KINONDONI AMTEMBELEA MUFTI MKUU WA TANZANIA OFISINI KWAKE

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi leo asubuhi ametembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abuubakar Zubeir ofisini kwake Kinondoni jijini Dar es salaam. Mkuu wa Wilaya na mufti wamezungumzia ushirikiano katika suala la kuhamasisha na kujenga ari miongoni mwa waumini kufanya kazi, kutunza mazingira, kulinda amani na utulivu, kuiombea nchi yetu, kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli pamoja na wasaidizi wake wote ili waweze kutimiza vema majukumu yao kwa taifa letu.
Mufti Mkuu wa Tanzania alimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa uamuzi wake wa kumtembelea na kumuahidi ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yake kwa wananchi kama Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA DKT ASHA_ROSE MIGIRO LEO OFISINI KWAKE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dkt Asha _Rose Migiro kabla ya Mazungumzo yao Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam Tarehe 19/05/2016
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan akiwa kaitka Mazungumzo na  na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dkt  Asha_Rose Migiro alipokwenda Ofisini kweke  leo Ikulu jijini Dar es Salaam Tarehe 19/05/2016


































































Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika Picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza  Dkt Asha_Rose Migiro leo Ikulu Dar es Salaam Tarehe 19/05/2016

MATUKIO MBALIMBALI BUNGENI DODOMA LEO

 Naibu Waziri wa Tamisemi, Seleman Jaffo akijadiliana jambo na Mbunge wa Busokelo, Atupele Mwakibete kwenye viwanja vya Bunge, mjni Dodoma. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Waziri Mkuu akijibu maswali ya wabunge , bungeni mjini Dodoma
 wabunge wakijadiliana jambo bungeni



new
 Wageni wakifuatia mwenendo wa Bunge

 Mbunge wa Jimbo la Ilemela,Anjelina   akijibu swali
 Spika wa Bunge akitoa pole kwa familia za waumini waliouwa msikiti jijini Mwanza na watu wasiojulikana waliokuwa wamevalia kininja
 Waziri Mkuu, Majaliwa kaizungumza na mmoja wa wabunge
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwasilisha hotuba ya makadirio ya Bajeti ya wizara hiyo.


NEW
NEW

NEW

NEW
NEW
Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, Ali Keisy akichangia majadiliano ya makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, bungeni Dodoma , ambapo aliutwatuhumu wapinzania wanaomsema vibaya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

NEW
 Mbunge wa Ulanga, Goodluck Ulanga  (kulia), akizungumza na Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo kwenye viwanja vya Bunge Dodoma.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwa na wanafunzi waliotembelea Bunge
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete akichangia hoja wakati wa majadiliano ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI MBALIMBALI PAMOJA NA KATIBU MTENDAJI WA SADC IKULU JIJINI DAR ES SALAAM














Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke Ikulu jijini Dar es Salaam.













Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke wakati wa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

 














Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke akimkabidhi Kitabu kinachohusu masuala mbalimbali ya Ujerumani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Ikulu Balozi wa Uturuki hapa nchini Yasemin Aralp aliyefika kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Denmark hapa nchini Eina Hebogrd Ikulu jijini Dar es Salaam.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Denmark hapa nchini Eina Hebogrd mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax Ikulu jijini Dar es Salaam. Dkt. Stergomena alifika Ikulu kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax pamoja na Maafisa wengine kutoka Ikulu na  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa. 





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax pamoja na Maafisa wengine kutoka Ikulu na  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.
TAARIFA YA CCM KUKANUSHA UZUSHI WA VYOMBO VYA HABARI.

TAARIFA YA CCM KUKANUSHA UZUSHI WA VYOMBO VYA HABARI.

sendeka

Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinatoa taarifa potofu kuhusu mchakato wa Mwenyekiti wa sasa wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti cha uongozi wa CCM kwa Rais John Pombe Magufuli kama ilivyo mila na desturi ya Chama Cha Mapinduzi.
Yamekuwepo madai eti Mwenyekiti amekataa au anachelewesha kukabidhi kijiti.
Habari hiyo sio kweli kabisa na ni kinyume chake, kwani Dkt. Kikwete amekuwa akisisitiza kukabidhi madaraka mapema iwezekanavyo. Kwa ajili hiyo kwenye kikao cha Mei 3, 2016 alikataa kusiongezwe agenda nyingine ambazo zitalazimisha Mkutano Mkuu Maalum kuchelewa kufanyika kwa sababu ya kukamilisha maandalizi ya agenda hizo. Alisisitiza agenda iwe moja tu.
Dhamira ya kufanyika Mkutano Mkuu maalum mwezi Juni, 2016 iko pale pale. Kilichoelezwa kwenye kikao ni kutaka kukamilisha utaratibu wa kupata fedha za kugharamia mkutano huo. Taratibu zikikamilika tarehe itapangwa. Mipango ya kutafuta pesa inaendelea na ikikamilika tarehe itatangazwa.
Tunawataka wana-CCM wasihamanike wala kubabaishwa na taarifa za upotoshaji zinazofanywa na watu wenye nia mbaya na CCM. Hawa ni wale wale ambao wamekuwa wakiiombea mabaya CCM bila ya mafanikio.
Pia tunapenda kukanusha madai ati kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwatahadharisha Wajumbe wa Kamati Kuu kuhusu ukimya wa Ndugu Edward Lowassa. Hakuna wakati wowote kauli kama hiyo aliitoa. Ni uzushi mtupu. Jina la Ndugu Lowassa halikutajwa kabisa.
Aidha, tunapenda kukanusha madai ya kufanyika mkutano baina ya Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa CCM kuhusu uchaguzi wa Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM. Hapajawahi kufanyika mkutano wa aina hiyo siku yoyote na mahali popote. Hivyo madai ya kuwepo kwa tofauti baina ya Viongozi wakuu kuhusu nani achaguliwe kuwa Katibu wa Wabunge wa CCM hayana msingi wowote.
Kamati Kuu iliteua Wabunge wanne kugombea na kuwaachia Wabunge wa CCM kuamua. Kuhusisha Viongozi na hasa kuzua kuwepo kutokuelewana ni jambo la kusikitisha.  Ni taarifa ya uongo yenye nia ovu kwa CCM na Viongozi wake.
Tunapenda kuwatahadharisha waandishi wa habari kuandika habari za ukweli. Waache kuzua mambo yenye kupandikiza chuki na mgawanyiko usiostahili kuwepo ndani ya CCM na kuyaeneza kwa watu. Waheshimu maadili ya kazi zao.
Napenda kuwahakikishia na kusisitiza kuwa hakuna mgogoro wa kukabidhi kijiti cha uenyekiti katika CCM na wala hautakuwepo.

Imetolewa na;


Ndugu Christopher Ole Sendeka   
                  MSEMAJI WA CCM                  
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
05/05/2016
MHE. DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA WATANZANIA NA WANACHAMA WA CCM WAISHIO JIJINI BEIJING โ€“ CHINA.

MHE. DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA WATANZANIA NA WANACHAMA WA CCM WAISHIO JIJINI BEIJING – CHINA.

sule
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe 20th April 2016 amekutana na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Tawi la Beijing ambao ni Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, katika Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State Guesthouse jijini Beijin, nchini China.
Wakisoma risala yao, Wanafunzi hao kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo Beijin na miji ya karibu kama vile Tianjin walimuhakikishia Mheshimiwa Dkt. Kikwete kuwa wao ni waaminifu na wazalendo kwa Taifa lao na kwamba wako tayari kurudi nyumbani na kutumia elimu zao katika kuhakikisha kuwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanafikiwa.
Katika mazungumzo na Wanachama hao, Mhe Kikwete amewakumbusha jukumu kubwa lililo mbele yao la kujenga Chama na kulijenga Taifa la Tanzania, katika hotuba yake ameeleza kuwa China imefanya Mapinduzi makubwa katika maendeleo na kuboresha ustawi wa watu wa nchi hiyo, hivyo kuwataka kujifunza na kuchukua maarifa ya China na kuyatumia wakirudi nchini ili kufanikisha Mapinduzi makubwa ya Kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.

Mheshimiwa Kikwete na Ujumbe wake wanatarajia kutembelea Jimbo la Fu Zhou hapo kesho na kushuhudia maendeleo makubwa yaliyosimamiwa na Katibu Mkuu wa CCP na Rais wa Serikali ya watu wa China Mhe Xi Jinping, pamoja na kufanya mazungumzo muhimu na Viongozi wa Chama Cha Kikomunisti cha China {CCP} katika jimbo hilo.
MWENYEKITI WA CCM NA RAIS MSTAAFU MHE. DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA FAFU

MWENYEKITI WA CCM NA RAIS MSTAAFU MHE. DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA FAFU

chuo4
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo Aprili 23, 2016 ametembelea Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha jimbo la Fujian (Fujian Agriculture and Forest University-FAFU) kilichopo katika mji mkuu wake Fu Zhou, China.
Mwenyekiti alikaribishwa chuoni hapo kuonyeshwa hatua ambazo jimbo hilo imepiga katika kuendeleza kilimo cha kisasa, teknolojia ya kuzalisha mbegu na teknolojia ya kupambana na magonjwa na wadudu waharibio mazao. Akiwa chuoni hapo, alikutana pia na wanafunzi wa kitanzania wanaosomea shahada za uzamivu kwa ufadhili wa serikali ya China.
Katika mazungumzo yake na Mkuu wa Chuo hicho Profesa Lan Siren, Mhe Kikwete amependekeza kuanzishwa kwa mahusiano na ushirikiano baina ya Chuo Cha Kilimo SUA na Chuo hiko. Pia amependekeza wanafunzi na wakufunzi wa chuoni hapo kuja Tanzania kufanya mafunzo ya vitendo na tafiti zao.
Kufuatia pendekezo hilo, Rais wa Chuo hicho ameelezea utayari wa Chuo hicho kushirikiana na SUA. Aidha, ameelezea  kulipokea ombi la Mwenyekiti la kuongeza nafasi za masomo kwa vijana wa Tanzania na kuahidi kulifanyia kazi ombi hilo.
Chuo Kikuu cha FUFA kina takribani wanafunzi elfu arobaini (40,000) ambapo wanafunzi kutoka Afrika ni takribani 120 kati yao watatu tu (3) wanatoka nchini Tanzania.
Mhe Kikwete yuko nchini China kwa ziara ya kichama iliyotokana na mualiko rasmi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China Mhe Xi Jinping.

MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA WAKUTANA NCHINI ZIMBABWE.

SGs 7

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akitoa mada kwenye Kongamano la siku Nne la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls Zimbambwe lilianza tarehe 4 – 8 Mei, 2016. Vyama hivyo ni ANC ya Afrika Kusini, FRELIMO ya Msumbiji, MPLA ya Angola, SWAPO Party ya Namibia na CCM ya Tanzania.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akimpongeza Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF Ndugu Ignatius Morgen Chombo kwa kufanikisha Kongamano  la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika na anaeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu wa FRELIMO Ndugu Eliseu Machava. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016
Picha ya pamoja ya Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) wanaoshiriki Kongamano la siku Nne la kutafakari uimarishaji na uendelezaji wa ushirikiano wao na namna ya kukabiliana na changamoto walizonazo. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini Ndugu Ndugu Gwede Mantashe, Katibu Mkuu wa FRELIMO ya Msumbiji Ndugu Eliseu Machava, Katibu Mkuu wa CCM ya Tanzania Ndugu Abdulrahaman Kinana, Makamu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomnisti cha China (CPC) Ndugu Guo Yezhou, Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF ya Zimbabwe Ndugu Ignatius Morgen Chombo, Katibu Mkuu wa MPLA ya Angola Ndugu Juliao Mateus Paulo na Katibu Mkuu wa SWAPO Party ya Namibia Ndugu Nangolo Mbumba. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini, Ndugu Gwede Mantashe kwenye Kongamano la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) linalofanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA KUU LA UWT TAIFA DODOMA.

IMG_6624

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wenye lengo la kukumbushana katika majukumu ya kiutendaji kwenye ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi hiyo Kuu  ya kitaifa. Mkutano huo umefunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Semina ya Mafunzo kwa ajili ya kuwajengea Uwezo Viongozi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM iliyofunguliwa leo Mei 7,2016 katika ukumbi wa MORENA Mjini Dodoma.
BABATI WAIPONGEZA CCM KWA KUMWAMINI NA KUMUUNGA MKONO RAIS DK. JOHN MAGUFULI KATIKA UPASUAJI MAJIPU

BABATI WAIPONGEZA CCM KWA KUMWAMINI NA KUMUUNGA MKONO RAIS DK. JOHN MAGUFULI KATIKA UPASUAJI MAJIPU

John_Magufuli_2015 (1)
WANANCHI mkoani Manyara wamekipongeza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kumwamini na kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli, kwenye jitihada zake za kurudisha nidhamu ya watumishi wa sekta za umma tangu alipoingia madarakani Novemba, 2015.
Pia wamekipongeza kwa kutambua uwezo alionao Christopher Ole Sendeka, ambaye ameteuliwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete, kuwa Msemaji wa Chama hicho ngazi ya Taifa.
Wakizungumza na kwa nyakati tofauti jana, wananachi hao wa wilaya ya Babati vijijini walisema wao ni mashuhuda wa namna CCM inavyoendelea kuimarika tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Walisema wanaamini ukomavu wa kidemokrasia ulioko ndani ya CCM ambao ulitumika kumpata Dk. John Magufuli ambaye aliipeperusha vema bendera ya chama kwenye uchaguzi huo uliokuwa wa kihistoria ni moja ya sababu za kurudi kwa uhai wa chama.
Paul Deemay mkazi wa kijiji cha Bashnet wilayani humo, alisema uhai huo umetoa matumaini mapya kwa wananchi kukiamini Chama hicho, kuwa ndicho chenye uwezo wa kuivusha Tanzania kwenda kwenye uchumi endelevu wa viwanda.
Alisema CCM ina utajiri wa viongozi makini wenye maono, sifa ambazo zinaendelea kudhihirika kutokana na kuwa na serikali yenye msimamo iliyoundwa Dk. Magufuli, ilani ya chama iliyokusudiwa kupambana na ufisadi na ukuzaji uchumi kwa kasi ya ajabu.
Naye Mary Focus, ambaye ni Mwanafunzi wa chuo cha kodi cha Dar es Salaam na mkazi wa Babati, alisema anatarajia mambo makubwa kwa Awamuhii ya Tano inayoongozwa na Dk. Magufuli asiyependa mzaha kwenye utumishi za umma.
Alisema Ole Sendeka aliyeteuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa CCM hivi karibuni ni mtu mchapakazi na kwamba mkoa wa Manyara unajivunia mafanikio yake kwenye siasa hivyo CCM imefanya chaguo sahihi kumpa jukumu hilo.
“Ole Sendeka anastahili kushika nafasi aliyokabidhiwa na CCM, ni mchapakazi na sisi watu wa Manyara na Tanzania kwa ujumla tu mashahidi katika hilo naamini atakitetea chama kwa akili na busara zake zote,”alisema Mary.

Kategori

Kategori